+ Add Song Image
SONG MR-PRESIDENT ARTIST R.O.M.A PRODUCER J-RIDER + YUDDI STUDIO TONGWE RECORDS romabraq@yahoo.com INTRO By…..Mwl. Julius Kambarage Nyerere Ikulu ni mahali patakatifu, ikulu ni mahala patakatifu, Mimi sikucha guliwa na wananchi wa Tanzania Kuja kupageuza kuwa pango la walanguzi Claps claps claps By…Roma Drop drop drop drop drop yop Haaa haaa… yes Surprise …Tongwe records We are here for revolution wooord Mr. president ..welcome to white house Thank you….aaaah …thank you ….yeaaah VERSE….1 Mi ndo’ roma mkatoliki mwenye asili ya kiyahudi Mpare wa milimani sa lamu ya kikwetu urewedi We ni mkwere wa chalinze ambaye hutamsahau mnyakyusa...(Mwakyembeee) Aliye wafundisha monduli siasa Aliyekula kiapo kwa agano jipya la wakorintho Siyo msabato mwenye siasa za kubattle kama Zitto Mwenye wito wa Appocalypto husssle za Kambikatoto Msaka ndoto kama kristo shujaa kama Mrisho Mpoto Jasiri kama Mandela busara kama Nyerere Niliyejificha mapangoni mithili ya Otango Osale So usinidanganye kwa uchawi waaa kutumia ndulele Au vita vya majimaji nife kama Kinjekitile Hatutaki siasa za kale, siku hizi tunawahi kubalehe Nawapa pole wakazi wote wa Tandale kwa Mtogole Akhsante Sheikh umeniita ikulu sio kisa nina nyota ya mshale Najua mvi sio busara ila naomba amani itawale Ikulu yako ina thamani zaidi ya falme za kiarabu Cha ajabu hawaithamini na inapoteza thawabu Taifa lilikutabri tangu enzi ukiwa waziri J.K wa 2 utakuja ongoza hii serikali Yenye vilio kote kama kina mama wa Galilaya Wanaoutafuta ukombozi wasimamishe Pobilahaya Viongozi wetu ni mafia na mabeautifull lier Nilikuwa na ndoto hizo ila bado hawaja niinspire CHORUS Pagani si mlituahidi mtamwaga na lami vipiii?...Badoooo Wanafuzi mlituahidi walimu mtawaleta!!...woooh Morogoro na Tanga vipiii?Badooo Dodoma…?Badooo… Kigoma…?Badooo.. Maisha bora kwa watanzania nyie wenyewe mlituambia Manurse…?Badooo Mapolice…?Badooo Ajira kwa vijana na maendeleo kwa kina mama Watotoo…?Badooo Kina mamaaa…?Badoooo VERSE….2 Inafahamika ulipewa nchi angali imeshachafuka Uongoze hii familia kubwa ya kizazi cha nyoka Na ukakubali kubeba huu msalaba wa ukombozi Hizi kashfa ndo’ changamoto zisikutoe machozi Sitosahau campaign zako za mwaka 2005 Nilichomwa na jua nikingoja upite nipunge mkono Traffic aliyepangwa saa moja kisha ukapita saa saba Akiwa na stress za mwanae shuleni kafukuzwa ada Leo mna nyumba mna mashamba mna viwanja mna viwanda Mi nasaga na rhumba na mshahara wangu haujapanda Yule traffic maisha magumu aaah muogopeni Mungu Nikisema it is not fair mnataka mnifunge pingu Gerezani kesi za wanyonge cheki zinapigwa tarehe Jamhuri itafata mkondo ee mola wangu wasamehe Wasaliti kama Eskarioti mbele ya Yesu Mnazarethi Wa sakramenti ya ekaristi bado hawaitaki torati!! Harakati ndo’ jadi siogopi hadi wanichape mjeledi Hadi yuddi alikuwa shahidi kwa vinanda na vinubi Elimu yetu bahati nasibu kama mikopo ya desi Kimbilio la waliofeli ni ualimu na upolisi Wamefisadi tenda ya rada, ndege ya raisi, magari ya jeshi Wote matraitor sasa skrepa kama Lubumbashi Wanapata alama za juu kwa kumuhonga penzi professor Mtunza pesa wa benki kuu kumbe pepa zote alidesa Au unataka 2010 mapinduzi yawe ya Liberia Eti utajiri ni mbuga, milima na ziwa Vicktoria Piga vita ujinga, umasikini na H.I.V carriers Askofu kutawala nchi hatutaki hizo elimu dunia Migomo ya chuo kikuu naitupia jicho la 3 Sitetei mpaka Rutashoborwa akiwa wakili kisutu Kul - nafs - dhal - kal - maut inasema torati Rest in peace shusha bendera ipepee nusu mlingoti Bungeni hawaijadili bajeti ya mlala hoi Mtu hataishi kwa mkate bali neno siyo divai Tazama timu yako iliyoko madarakani Na mchunguze kwa makini anayelia sana msibani. CHORUS Walimu si mlituahidi mtatupa hela zetu vipiii…?Badooo Mitihani si mliahidi haitavuja tena….woooooh Nachingwea na Mbeya vipiii…?Badooo Tabora…?Badooo Mtwara…?Badooo Maisha bora kwa watanzania nyie wenyewe mlituambia Wamachinga…?Badoooo Wakulima…?Badooo Ajira kwa vijana na maendeleo kwa kina mama Wazee…?Badooo Vyuo vikuu…?Badooo VERSE….3 Huu sio wakati wa kuwaua maalbino Angalau mapinduzi kama Macio Maximo Usihangaike kumtafuta Roma…mi!! Hakimu wa getho Mwenye sauti ya mamlaka!!! iliyomfikisha Mrombo Keko Baada ya kukemea ufisadi na sera za Karamagi Na waliokula jasho letu kwenye migodi ya Buzwagi Utazuia vipi ongezeko la wimbi la ukeketaji… Wakati Ngariba ndo’ diwani wa kata kwenye kijiji!! Neither do I…!! hongera ulipima ukimwi Watanzania nasi tuamke tusimpige kibao tu Mwinyi Hapa nagundua aya-tul - munafik - thalatha Inawezekana aliishia alifu wakati anasoma madrasa Huu sio muda wa kujadili kesi za Manji na Mengi Hayo ya Mungu we Kaisari jadili mambo ya msingi Teacher alipojiita mtabiri Tanganyika wote vipofu Padre wa kwanza pentekoste ubatizo wa maji marefu Machozi yalinitoka Segera watoto hawapati haki Wengi wamekimbia shule basi lije wauze visheti Wanaosomeshwa kwa mtaji wa chapati na uvuvi wa samaki Wabunge wao wamekaa na wanajiita wanaharakati!! Rudi kwenu kahamasishe nduguzo hawana taaluma Wazaramo wamegoma soma still mwali wanamcheza ngoma Wanalia Kilwa Kivinje huku wanaocheka ni wabunge Walionunua kura ya bibi kwa kumuhonga doti ya kitenge Hata wamasai walikuchagua kwa kura nyingi za upendo Wakiamini mtetezi yuaja wa jimbo la Oldoyo Sambo Waambie what is going on ndani ya himaya ya bwawa la Mtera Waonyeshe na mikataba ya utawala wa mgodi wa Kiwira Jeshi lote kwenda Tarime hawakuwa na njia mbadala Na walioteketea Mbagala!! Mr.pres …. Haya masikharaaaa!!! Sina maana utoke wewe hicho kiti umuachie professor Nisamehe kama nakosea maana mimi sio mwanasiasa Claps claps claps OUTRO By…Mwl...Julius Kambarage Nyerere Kwa hiyo kitu kimoja tunataka kuelewa… ni hali ya matatizo ya nchi yetu yalivyo sasa hivi....Eee!! Kwasababu...sera ya...ay..…awamu ya kwanza…. awamu yangu mimi… imefanya mema…. imefanya ya kijinga…. ya kijinga yanaachwa…!! lazima yaachwe…. Ubaya wenu ni kwamba…. mnaacha mema...mnachukua ya kijinga.
© 2006-2025 BandLab Singapore Pte. Ltd.
All third party trademarks are the property of the respective trademark owners. ReverbNation is not affiliated with those trademark owners.